Higher Education Students' Loans Board
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza orodha ya majina ya wanafunzi 640 wenye ufaulu wa juu katika mitihani ya kidato cha sita (ACSSE) ya mwaka 2023 katika tahasusi za sayansi waliodahiliwa katika Vyuo vya Elimu ya Juu kwenye fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) kwa mwaka 2023/2024 ambao wamependekezwa kunufaika na ‘Samia Scholarship’.
Wanafunzi husika wanashauriwa kutembelea tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia www.moe.go.tz au kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz kusoma majina yao kwenye orodha na kukamilisha taratibu za kuomba Ufadhili wa ‘Samia Scholarship’ kupitia mfumo https://olas.heslb.go.tz kabla ya dirisha kufungwa tarehe 15 Oktoba, 2023.
Ili kuona majina bofya hapa