Higher Education Students' Loans Board
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ( HESLB), Dkt Bill Kiwia leo ameanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara.
Baada ya kuwasili mkoani hapo alifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala kumsalimu pamoja kumwelezea mafanikio ya taasisi hiyo hususan katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Aidha, katika ziara hiyo, ambayo ameambatana na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa HESLB, Dkt. Kiwia anatarajiwa kukutana na wanufaika na waajiri walioko mkoani Mtwara.