Higher Education Students' Loans Board
Tunapenda kuufahamisha umma na wanufaika wote wa mikopo ya elimu ya juu kuwa kumekuwepo na upotoshaji kutoka kwa ‘matapeli’ wanaowaelekeza wanufaika kulipa madeni yao kupitia akaunti za benki za watu binafsi.
Tunawaasa wanufaika wote kupuuza taarifa zinazotolewa na watu binafsi na badala yake kufuata utaratibu rasmi wa malipo ya HESLB.
Kupitia taarifa hii, tunakumbusha kuwa malipo yote ya mikopo hufanyika kupitia namba ya malipo (Control Number) ya mnufaika inayotolewa na HESLB na inayoonekana kwenye ankara ya deni (Loan Statement) ya mnufaika. HESLB haina wakala na haipokei malipo kupitia akaunti ya benki ya mtu binafsi.
Namna ya kupata Control Number ili kulipa deni lako:
1. Tembelea tovuti ya HESLB: www.heslb.go.tz
2. Ingia kwenye mfumo wa wanufaika (Repayment Portal)
3. Jisajili kwa kutumia taarifa zako (Form Four Index Number)
4. Pata taarifa ya deni lako (Loan Statement) yenye Control Number kwa ajili ya malipo
5. Lipa kupitia benki au simu ya mkononi
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Simu: 0736 66 55 33, ujumbe wa WhatsApp: 0739 66 55 33 au barua pepe: info@heslb.go.tz
Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
Ijumaa, Septemba 5, 2025