Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


31
August 2025

TAREHE YA MWISHO YA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO 2025/2026 YASOGEZWA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha Waombaji wa mikopo na Umma kwa ujumla kuwa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha  maombi ya mikopo imesogezwa mbele kutoka tarehe 31 Agosti hadi tarehe 14 Septemba, 2025.

Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kuwasilisha maombi ya mikopo katika muda uliokuwa umepangwa.

Hadi kufikia leo, tarehe 31 Agosti, 2025, jumla ya maombi ya mikopo 157,309 yameshapokelewa kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Idadi hiyo ni ongezeko la 5% ikilinganishwa na maombi 150,530 yaliyokuwa yamepokelewa katika  kipindi kama hiki mwaka jana, 2024/2025.  Aidha, maombi 960 ya ‘Samia Scholarship’ yameshapokelewa ikilinganishwa na maombi 742 yaliyokuwa yamepokelewa  mwaka 2024/2025, ikiwa ni ongezeko la 29%.

Itakumbukwa kuwa, Bodi ilianza kupokea maombi ya mikopo ya wanafunzi kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 15 Juni, 2025.

Kupitia tangazo hili, waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2025/2026 ambao wamejisajili lakini hawajakamilisha, wanashauriwa kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa.

Bodi inapenda kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 14 Septemba, 2025.

 

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Jumapili, Agosti 31, 2025