Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


1
August 2025

Viongozi wa ZHESLB Watembelea HESLB

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar (ZHESLB) Prof. Mohammed Hafidh akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji  wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar (ZHESLB) Bi Umrat Mohammed leo wametembelea Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) zilizopo eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam.

Prof. Hafidh alifika kumtambulisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa ZHESLB ambaye ameteuliwa kushika wadhifa huo na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi mwezi Machi mwaka huu. 

Viongozi hao wawili wa ZHESLB wamepokelewa na Menejimenti ya HESLB ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Bill Kiwia.