14
Nov 2026

TAARIFA KWA UMMA

  • Wanafunzi 46,435 wapangiwa Mikopo ya TZS 148.03 bilioni
  • Wamo waliokata rufaa

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya wanafunzi 46,435 ambao wamepangiwa mikopo na ruzuku yenye thamani ya TZS 148.03 bilioni kwa mwaka wa masomo 2026/2027 wakiwemo wanafunzi 1,807 wa mwaka wa kwanza ambao wamepangiwa mikopo baada ya rufaa zao kufanikiwa.

Mikopo kwa Wanafunzi wapya na wanaoendelea

Taarifa iliyotolewa leo (Ijumaa, Novemba 13, 2026) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, imesema kuwa wanafunzi 15,374 ni wa mwaka wa kwanza ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 48.24 bilioni.

Wanafunzi 25,371 wa mwaka wa pili na kuendelea ambao  wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 80.64 bilioni. Aidha, taarifa hiyo ya Dkt. Kiwia inataja idadi ya wanafunzi 5,422 wa mwaka wa pili na kuendelea ambao wamepangiwa mikopo kwa mara ya kwanza yenye thamani ya TZS 17.67 bilioni.

Samia Scholarship

Kwa upande wa ruzuku ya Samia Scholarship, wanafunzi 37 wapya wamepangiwa ruzuku yenye thamani ya TZS 188.12 milioni na 231 wanaoendelea na masomo wamepangiwa ruzuku yenye thamani ya TZS 1.29 bilioni.

Hitimisho

Kwa taarifa hii, wanafunzi ambao hawakupangiwa mikopo kwa sababu mbalimbali, wanashauriwa kuomba dirisha litakapofunguliwa kwa mwaka wa masomo 2027/2028.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji,

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Ijumaa, Novemba 13, 2026

Taarifa hii pia inapatikana kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii (Facebook na Instagram) kwa jina la HESLB Tanzania.

Published: November 14, 2026 at 8:40 AM