Loan Repayment FAQs
HESLB loan repayment section
Popular Questions
Je deni la HESLB linalipika?
- LINALIPIKA: Na kwa wastani, kila mwezi wanufaika 240 wanamaliza madeni yao
- Wanufaika wote wa mikopo WANAKUMBUSHWA kujitokeza na kuanza kurejesha kwa wakati ili kuweza kusomesha Watanzania wengine wahitaji
Kikokotoo cha makato ya HESLB kikoje?
- Mnufaika aliyeajiriwa anapaswa kukatwa 15% tu ya mshahara wake
- Ikiwa mshahara wake ni TZS 1,000,000.00 atakatwa TZS 150,000.00 (15%) tu
General Questions
Mwajiri anapaswa kufanya nini baada ya kuajiri wahitimu wapya?
- Kwa mujibu wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (SURA 178), mwajiri anapaswa aijulishe Bodi kwa maandishi kuhusu waajiriwa wapya ambao ni wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu ndani ya siku 28 tangu tarehe ya kuajiriwa
Ni lini mnufaika wa mkopo anapaswa kuanza kurejesha mkopo wake?
- Mkopo huanza kulipwa inapomalizika miezi 24 baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya juu au baada ya kusitisha masomo kwa sababu yoyote ile
Mnufaika wa mkopo anapaswa kufanya nini ili kulipa deni lake?
- Mara baada ya kuhitimu masomo au kusitisha masomo yake kwa sababu yoyote ile, mnufaika anapaswa aitaarifu Bodi kwa maandishi mahali alipo na hali ya ajira yake na kuanza kurejesha mkopo wake
Makato huwasilishwaje HESLB?
- Kwa wanufaika waajiriwa, hukatwa asilimia kumi na tano (15%) ya mshahara wa kila mwezi
- Mnufaika aliyejiajiri anapaswa kurejesha kiwango cha chini cha shilingi 100,000/= kila mwezi