10
Feb 2026

ZHESLB Yaikabidhi Tuzo HESLB kwa Kuchangia Mafanikio Yake

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Bill Kiwia leo (Jumanne, Februari 10, 2026) amepokea tuzo kwa kutambua ushirikiano anaoutoa kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar (ZHESLB) katika kufanikisha utendaji na mafanikio waliyofikia.

Dkt. Kiwia ameshiriki katika hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi kati ya ZHESLB na Maafisa Mikopo wa Vyuo Vikuu na vya Kati kinachofanyika Mkoa wa Kusini Pemba.

Kikao hicho kimefunguliwa na Mhe. Rashid Hadid Rashid, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba akimwakilisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Leila Mohammed Mussa.

Aidha, maafisa mikopo wapatao 120 kutoka vyuo vikuu na vya kati vya Tanzania Bara na Visiwani wanahudhuria katika kikao hicho Kikao kazi hicho cha siku tatu kilichoanza leo tarehe 10 Februari na kitafikia tamati tarehe 12 Februari, 2026.

HESLB na ZHESLB zimekuwa zikishirikiana katika masuala ya kiutendaji na ziliingia katika mashirikiano rasmi mnamo mwezi Aprili mwaka 2021.

Published: February 10, 2026 at 7:10 PM