Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza orodha ya wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo kupitia mpango wa ‘Samia Scholarship’ kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
Ufadhili huo umetolewa kwa wanafunzi 1,000 waliopata ufaulu wa juu katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita unaosimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika tahasusi za sayansi.
Wanafunzi hao watagharimiwa masomo yao ya shahada ya kwanza baada ya kuomba au kupata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba, kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB). Mwongozo huo unapatikana hapa.
Ili kuona majina ya wanafunzi waliopata ufadhili wa ‘Samia Scholarship’ kwa mwaka 2026/2027 bofya hapa