Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


18
June 2025

USAJILI WA TAASISI ZINAZOTOA UFADHILI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI NA STASHAHADA

- Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu wadau wote kuwa imeanza mchakato wa usajili wa taasisi na mashirika yanayotoa ufadhili kwa wanafunzi wanaosoma katika ngazi ya Sekondari na Stashahada.

- Lengo la usajili huu ni kuwezesha taasisi hizo kutambuliwa rasmi na Bodi ya Mikopo, na kuwa na utaratibu wa kubadilishana taarifa za wanufaika wao kwa lengo la kupewa kipaumbele pale watakapohitaji kugharimiwa masomo yao ya elimu ya juu kupitia HESLB

- Kwa maelezo kuhusu usajili na nyaraka zinazohitajika yanapatikana kwenye tovuti hii bofya hapa

- Iwapo unahitaji taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Bw. Godfrey Chawe (Meneja wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo) kupitia simu namba +255 714 266 811 au barua pepe: godfrey.chawe@heslb.go.tz

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Juni 17, 2025