Higher Education Students' Loans Board
WAMO WALIOPANGIWA KATIKA DIRISHA LA RUFAA
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Jumatatu, Disemba 01, 2025) imetangaza awamu ya tatu ya upangaji mikopo na ruzuku kwa mwaka 2025/2026 yenye jumla ya wanafunzi 21,851. Idadi hii inajumuisha mikopo iliyopangwa katika Dirisha la Rufaa na waombaji wapya wanaoendelea na masomo kama ifuatavyo:
- Wanafunzi 6,487 wa shahada ya awali wamepangiwa mikopo kupitia dirisha la rufaa kiasi cha TZS. 21.5 bilioni.
- Wanafunzi 2,611 wa shahada ya awali wamepangiwa mkopo kupitia maombi ya kawaida kiasi cha TZS. 8.3 bilioni.
- Wanafunzi 11,419 wanaoendelea na masomo (FTCs) wamepangiwa mikopo kwa mara ya kwanza yenye thamani ya TZS. 37.2 bilioni.
- Wanafunzi 1,235 wa stashahada wa mwaka wa kwanza wamepangiwa kiasi cha TZS. 3.2 bilioni
- Wanafunzi 31 wapya wa ‘Samia Scholarship’ wamepangiwa ruzuku kiasi cha TZS. 5 bilioni
- Wanafunzi 68 wa Shahada za Juu (Postgraduate Degrees), (53 Shahada ya Uzamili na 15 Shahada ya Uzamivu) wamepangiwa TZS. 361.7 milioni.
Bodi itaendelea kupanga mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo na kukamilisha malipo kwa wanafunzi ambao wamewasili vyuoni.
Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Jumatatu, Disemba 01, 2025
Taarifa hii pia inapatikana pia kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram – ‘HESLB Tanzania’.