Higher Education Students' Loans Board
WANAFUNZI WA STASHAHADA WALIOPANGIWA MIKOPO DIRISHA LA MWEZI MACHI 2025 WAFIKIA 1,413
Tunawataarifu wanafunzi wote walioomba mikopo na umma kwa ujumla kuwa jumla ya wanafunzi 1,413 walioomba mikopo dirisha la mwezi Machi, 2025, wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 3,388,017,500.00 hadi kufikia Ijumaa, tarehe 16 Mei, 2025.
Idadi hiyo, ni ongezeko la wanafunzi 540 kutoka wanafunzi 873 ambao tulitangaza kuwapangia mikopo yenye thamani ya TZS 1,944,922,500.00 katika taarifa tuliyoitangaza tarehe 5 Mei, 2025.
Katika mwaka huu wa masomo 2024/2025, jumla ya wanafunzi 9,144 wa stashahada wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 23,981,542,101.00 kati yao; wanafunzi wa mwaka wa kwanza ni 7,040 wenye mikopo ya jumla ya TZS 18,242,010,001.00 na wanafunzi wanaoendelea ni 2,104 wenye mikopo ya thamani ya TZS 5,739,532,100.00
Kupitia taarifa hii, upangaji wa mikopo kwa mwaka 2024/2025 umekamilika kwa wanafunzi wa stashahada.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Jumamosi, Mei 17, 2025