Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


3
January 2024

STASHAHADA TATU, AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI ZAONGEZWA MIKOPO YA ELIMU

Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wa stashahada (Diploma) katika fani za Afya na Sayansi Shirikishi (Health and Allied Sciences) kuwa Serikali imeongeza wigo wa wanafunzi wa stashahada wanaonufaika na mikopo ya elimu.

Fursa zilizoongezwa ni kwa wanafunzi wa stashahada tatu mpya ambazo ni Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira (Ordinary Diploma in Environmental Health Sciences); Stashahada ya Kumbukumbu ya Taarifa za Afya na Teknolojia (Ordinary Diploma in Health Records and Information Technology); na Stashahada ya Sayansi ya Maabara (Ordinary Diploma in Medical Laboratory Sciences’).

Hivyo, kuanzia Januari 2, 2024, wanafunzi wa stashahada hizi ambao wapo katika mwaka wa kwanza na wanaoendelea wanaweza kuomba mkopo wa elimu.

Aidha, wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu, wanashauriwa kwa umuhimu mkubwa, kusoma ‘TOLEO LA PILI’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’. Mwongozo huu unapatikana katika www.heslb.go.tz

Mwongozo huu, pamoja na mambo mengine, unaeleza sifa na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mkopo kwa njia ya mtandao kupitia https://olas.heslb.go.tz

 

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Jengo la PSSSF, Barabara ya Makole,

S.L.P. 984,

DODOMA

Jumatano, Januari 3, 2024