Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


21
December 2023

DIRISHA MIKOPO YA STASHAHADA LAFUNGULIWA AWAMU YA PILI

Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi na umma kuwa dirisha la kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kutoka kwa wanafunzi wa stashahada (diploma) kwa mwaka wa masomo 2023/2024 limefunguliwa kwa awamu ya pili kwa siku 14 kuanzia leo, Alhamisi, Disemba 21, 2023.

Awali, dirisha la kupokea maombi ya mkopo kutoka kwa wanafunzi wa stashahada lilifunguliwa Novemba 7, 2023 na awamu ya kwanza ya wanafunzi waliopangiwa mikopo ilitangazwa na kusambazwa vyuoni Novemba 29, 2023.

Katika dirisha la awamu ya pili, wanafunzi walengwa wamegawanyika katika makundi matatu ambao watapaswa kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia https://olas.heslb.go.tz/olams/pre-applicant 

Kundi la Kwanza ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Stashahada za kipaumbele kama zilivyotajwa katika ‘TOLEO LA KWANZA’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’ ambao awali hawakuweza kuomba kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuchelewa hadi dirisha kufungwa.

Kundi la Pili ni wanafunzi wa mwaka wa pili au wa tatu wa Stashahada za kipaumbele kama zilivyotajwa katika ‘TOLEO LA KWANZA’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’. Wanafunzi hawa, ambao awali hawakuweza kuomba mkopo, sasa wanaruhusiwa kuomba.

Kundi la Tatu ni wanafunzi wa stashahada za kipaumbele ZITAKAZOONGEZWA siku chache zijazo kupitia ‘TOLEO LA PILI’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’. Stashahada zitakazoongezwa zitatangazwa kupitia tovuti www.heslb.go.tz kabla ya Disemba 23, 2023.

Tunawakumbusha wanafunzi wote wanaoomba mkopo wa Stashahada kupitia dirisha hili la awamu ya pili kusoma ‘TOLEO LA KWANZA’ la ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024’ ambao unapatikana katika www.heslb.go.tz na www.nactvet.go.tz

 

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Jengo la PSSSF, Barabara ya Makole,

S.L.P. 984,

DODOMA

Alhamisi, Disemba 21, 2023