Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


6
July 2022

DIRISHA LA KUOMBA MKOPO KUFUNGULIWA KABLA YA JULAI 15

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) linapenda kuwataarifu wanafunzi na umma kuwa inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2022/2023 na dirisha litafunguliwa kabla ya Julai 15, 2022.

“Taarifa hii inatolewa kufuatia maombi mengi ya taarifa ya ufafanuzi kutoka kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka 2022 na matokeo yao kutangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), jana, Jumanne Julai 5, 2022.” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru leo (Julai 6, 2022).

Kwa sasa, waombaji mkopo watarajiwa wanashauriwa kuwa watulivu na kuanza maandalizi ya awali ya kuandaa nyaraka muhimu kama vyeti vyao vya kuzaliwa au vyeti vya vifo vya wazazi wao vilivyohakikiwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na Wakala wa Usajili wa Matukio Muhimu Zanzibar (ZCSRA).

Aidha, maelezo ya kina kuhusu sifa na utaratibu wa kuomba mkopo kwa mwaka 2022/2023 yatapatikana katika ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa mwaka 2022/2023’ utakaoanza kupatikana katika www.heslb.go.tz kuanzia Julai 15, 2022.

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

DAR ES SALAAM

Jumatano, Julai 6, 2022