Higher Education Students' Loans Board
Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wa Stashahada (Diploma) waliopata udahili wa kuanza masomo mwezi Machi, 2024 kuwa dirisha la kuomba mkopo kwa njia ya mtandao litafunguliwa kwa WIKI TATU kuanzia Machi 1, 2024 hadi Machi 22, 2024.
Wanafunzi wanapaswa kusoma ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024 (TOLEO LA PILI)’ ambao unapatikana katika www.heslb.go.tz na www.nactvet.go.tz ili kufahamu kozi zinazopewa kipaumbele na utaratibu wa kuwasilisha maombi.
Kwa wanafunzi wa Stashahada waliodahiliwa awali na hawakuwa wamepata fursa ya kuomba mikopo, wanaruhusiwa pia kuomba mkopo kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyoorodheshwa kwenye mwongozo.
MUHIMU: Wanafunzi waombaji wanasisitizwa kuzingatia muda wa kuwasilisha maombi (Machi 1 - 22, 2024) kwa kuwa hautaongezwa ili kutoa fursa ya uchambuzi na upangaji mikopo kwa wenye sifa.
Imetolewa na;
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DODOMA
Alhamisi, Februari 29, 2024