Higher Education Students' Loans Board
Dodoma, Februari 22, 2024
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia aliyefika ofisini kwa Waziri jijini Dodoma kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa Februari 6 mwaka huu.
Katika kikao hicho, kilichohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Prof. Peter Msoffe, Prof. Mkenda ameelekeza, pamoja na mambo mengine, HESLB kuendelea kuzingatia sheria, sera na maelekezo ya Wizara na Serikali kwa ujumla katika kutekeleza majukumu yake.
Dkt. Kiwia aliongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB Prof. Hamisi Dihenga ambao wamemshukuru Prof. Mkenda kwa ushirikiano na miongozo anayoitoa kwa HESLB ambayo inaimarisha utendaji na kuongeza tija