Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


18
November 2023

UFAFANUZI: MALIPO YA FEDHA ZA MIKOPO HULIPWA AKAUNTI YA BENKI YOYOTE

Tunapenda kuwakumbusha wanafunzi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kuwa malipo ya fedha za mikopo inayotolewa na Serikali kupitia HESLB yanalipwa na kupokelewa na mwanafunzi-mnufaika kupitia akaunti yake ya benki aliyoichagua na kuisajili kupokelea fedha za mkopo wake.

Ufafanuzi huu unatolewa kufuatia maswali na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi wanufaika wa mikopo pamoja na viongozi wa Serikali za Wanafunzi.

Itakumbukwa kuwa, kupitia matangazo yetu kwa waombaji mkopo wa mwaka 2023/2024 yaliyotolewa kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba, 2023, tuliwasihi wanafunzi wote waombaji wa mkopo na wanufaika kufungua akaunti za benki katika taasisi za fedha za chagua lao.

Hivyo, ufafanuzi huu unalenga kuwakumbusha wanafunzi-wanufaika wa mikopo kuwa taratibu na mifumo ya malipo ya fedha za mikopo ya HESLB inaruhusu wanufaika wote kulipwa kwa wakati kupitia akaunti za benki mbalimbali walizozichagua.

Kwa ufafanuzi huu, tunawahakikishia wanafunzi wote wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu kutoka HESLB kuwa kila mnufaika aliyekamilisha taratibu za usajili chuoni na kwenye mfumo wa malipo wa HESLB (DiDiS) atalipwa fedha zake kwa wakati kupitia akaunti ya benki aliyoichagua.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji,

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),

Jengo la PSSSF, Barabara ya Makole,

S.L.P. 984,

DODOMA

#WeweNdoFuture

#TimizaWajibu