Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


8
July 2023

MAOMBI YA MIKOPO 2023/2024 KUANZA KUPOKELEWA JULAI 15

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwajulisha waombaji mikopo watarajiwa kuwa inakamilisha kuandaa mfumo ambao kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka huu 2023/2024 waombaji hawatahitajika kuwasilisha nakala ngumu (hard copies) na hivyo kuwapunguzia gharama za uombaji.

Dirisha la kuomba mkopo kwa njia ya mtandao litakuwa wazi kuanzia Julai 15, 2023.

Aidha, kabla ya kuanza kuomba mikopo Julai 15, 2023, HESLB itatangaza ‘Mwongozo wa Utoaji Mkopo na Ruzuku kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa Mwaka wa Masomo 2023/2024’ utakaopatikana katika tovuti www.heslb.go.tz. Waombaji wote wanashauriwa kuusoma na kuuzingatia.

 

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Jengo la PSSSF, Ghorofa ya Nne,

Barabara ya Makole,

S.L.P. 984,

DODOMA

Julai 8, 2023