Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


21
November 2022

HESLB YAPOKEA RUFAA 32,777 ZA WANAFUNZI WAOMBAJI MIKOPO

 

HESLB imepokea rufaa 32,777 za wanafunzi wahitaji wa mikopo ya elimu ya juu waliowasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia dirisha la rufaa lililofungwa jana Jumapili (Novemba 20, 2022).

Rufaa hizo ni maombi yaliyowasilishwa na wanafunzi wahitaji kutokana na kutoridhishwa na viwango vya mikopo waliyopangiwa na HESLB katika awamu mbalimbali za upangaji na utoaji mikopo katika mwaka wa masomo 2022/2023

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa vyombo vya habari leo Jumatatu Novemba 21, 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru amesema majibu ya rufaa hizo yatatangazwa (Jumamosi Novemba 26, 2022) na wanafunzi watapata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mkopo maarufu kama SiPA (Student’s Individual Permanent Account).

Kuhusu idadi ya Wanafunzi waliopangiwa kwa mwaka 2022/2023, Badru amesema kuwa hadi sasa jumla ya wanafunzi 166,438 tayari wamepangiwa mikopo, wakiwemo wanafunzi 68,460 wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wengine 97,978 wanaoendelea na masomo.

“HESLB inaendelea kupanga mikopo kwa wanafunzi wote wahitaji na kwa wale wanaoendelea na masomo tunavisisitiza vyuo kuendelea kutuma matokeo ya wanafunzi……Tumeendelea kupeleka fedha katika vyuo mbalimbali nchini” amesema Badru.

Katika hatua nyingine Badru amesema Serikali imeipaitia HESLB kiasi cha TZS 84 Bilioni zikiwa ni nyongeza ya fedha za bajeti ya fedha zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu katika mwaka 2022/2023 na hivyo kufanya bajeti itakayotolewa na Serikali kufikia TZS 654 Bilioni

“Ongezeko hilo limewezesha kuwapangia mikopo wanafunzi wanufaika wapatao 28,000. Tayari taarifa za kundi hili zinapatikana katika akaunti za SiPA na kuwasilishwa vyuoni kupitia awamu ya 4 & 5 kwa hatua za usajili na malipo.

Aidha Badru alisema HESLB inawasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa kupitia rufaa ukiendelea na wale waliopangiwa mikopo, taarifa zao zinapatikana kwenye SiPA na fedha zao tayari zimeshatumwa vyuoni.

Imetolewa na:

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

DAR ES SALAAM

Jumatatu, Novemba 21, 2022