Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


7
June 2022

KISHINDO CHA SIFURISHA AWAMU YA NNE KUTIKISA MIKOA 4

Kampeni ya SIFURISHA awamu ya 4 imeanza rasmi Jumatatu Juni 6, na itaendelea hadi Juni 24  mwaka ikiunguruma katika Mikoa 4 nchini pamoja na Zanzibar.

Mratibu wa SIFURISHA HESLB, Veneranda Malima ameitaja mikoa inayohusika katika awamu hii, kuwa ni pamoja na Kagera, Kilimanjaro, Njombe, Tabora na Zanzibar.

Malima amesema timu ya Maafisa wa HESLB wamejipanga vyema katika kutoa huduma bora kwa wateja na kuwataka wanufaika wa mikopo kufika katika maeneo husika ili kupatiwa huduma ikiwemo kupata taarifa ya deni la mkopo wa elimu pamoja na kumaliza deni la mkopo.

Mikoa itakayoanza ni Kagera, Kilimanjaro na Njombe kuanzia tarehe 6-10 Juni, Tabora tarehe 13-17 Juni, 2022 na baadaye Zanzibar tarehe 18-24 Juni mwaka huu” amesema Malima.

Kampeni ya SIFURISHA yenye lengo la kuhamasisha wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu kulipa mikopo yao hadi kuwa sifuri, imekwishafanyika katika mikoa 11 ambayo ni Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Geita, Dodoma, Zanzibar (Pemba), Tanga, Songwe, Morogoro, Shinyanga na Ruvuma.