Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


7
June 2022

BILIONI 570 KUKOPESHWA KWA MWAKA 2022/2023

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatarajia kutoa mikopo yenye thamani ya kiasi cha TZS 570 Bilioni kwa mwaka wa masomo 2022/2023.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2022/2023, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb) amesema Serikali kupitia itaendelea HESLB itaendelea kuratibu maombi, uchambuzi na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa na vigezo.

“Serikali imeendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya kugharimia Elimu ya Juu nchini kwa lengo la kuongeza fursa za upatikanaji wa Elimu ya Juu ili kuendana na mahitaji yanayotokana na ongezeko kubwa la uhitaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu” amesema Prof. Mkenda.

Aidha Prof. Mkenda amesema HESLB inatarajia kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika taasisi 19 za Elimu ya Juu katika ufundishaji, ujifunzaji na usimamizi kwa lengo la kuimarisha mazingira ya utoaji wa elimu katika ngazi hiyo.

Soma Bajeti ya Wizara ya elimu