Home

Main Menu

mega holdings

OLAS
Welcome

The Higher Education Students' Loans Board was established by Act No. 9 of 2004, inaugurated by the Hon. Minister for Higher Education, Science and Technology on the 30th March 2005 and became operational in July 2005. The objective of the Board is to assist, on a loan basis, needy students who secure admissions in accredited higher learning institutions, but who have no economic power to pay for the costs of their education. The Board is also entrusted with the task of collecting due loans from previous loan beneficiaries in order to have a revolving fund in place so as to make the Board sustainable.... Read More

MWONGOZO KWA WALIONUFAIKA NA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

1.0. UTANGULIZI

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 9 ya mwaka 2004 na ilianza kufanya kazi mnamo mwezi Julai mwaka 2005. Kwa mujibu wa sheria hii, baadhi ya majukumu makuu ya Bodi ni pamoja na kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika masomo ya shahada au stashahada ya juu katika taasisi za elimu ya juu zinazotambuliwa na Serikali hapa nchini na nje ya nchi.

Vilevile, sheria hii imeipa Bodi mamlaka ya kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu walionufaika na mikopo hiyo kuanzia mwaka 1994 ili pesa hizo ziweze kukopeshwa kwa wanafunzi wengine watakaohitaji.

2.0. UCHANGIAJI WA ELIMU YA JUU

Umuhimu wa kuanzishwa kwa Bodi hii ulitokana na sera ya serikali ya uchangiaji wa gharama katika huduma mbalimbali za jamii zilizoanzishwa katika miaka ya mwanzo ya 1990, ambapo mkondo mmojawapo katika sera hizo ulikuwa ni sera ya uchangiaji wa gharama za elimu ya juu.

Sera hii ya uchangiaji wa gharama za elimu ya juu iliandaliwa na kupangwa kutekelezwa katika awamu tatu kama ifuatavyo:

2.1. Awamu ya kwanza ilianza kutekelezwa mwaka 1992/93 ambapo wanafunzi walitakiwa kujilipia gharama za usafiri kwenda chuoni na kurudi nyumbani, gharama za udahili na usajili pamoja na michango ya serikali za wanafunzi. Gharama hizi zilikuwa ni ndogo na kila mwanafunzi aliweza kuzimudu.

2.2. Utekelezaji wa awamu ya pili ya sera hii ulihitaji mwanafunzi pamoja na kuchangia gharama zilizoainishwa katika awamu ya kwanza, alipie pia gharama za chakula na malazi. Gharama hizi ambazo kwa wakati huo zilifikia shs 350,000.00 kwa mwaka zilikuwa kubwa kwa wanafunzi walio wengi. Ili kuhakikisha kuwa kuna fursa sawa katika utoaji elimu ya juu, Serikali ilianzisha utaratibu wa mikopo ili wanafunzi ambao hawana uwezo wa kujigharamia waweze kukopeshwa moja kwa moja kutoka Serikalini. Utaratibu huu ulianza kutumika mwaka 1994/95 na uliendelea kutumika hadi mwaka 2004/2005.

2.3. Awamu ya tatu ilianza kutekelezwa mwaka wa masomo 2005/06 baada ya kuanzishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa Sheria Na. 9 ya mwaka 2004. Awamu ya tatu inamtaka mwanafunzi agharamie pamoja na gharama zilizotajwa kwenye awamu ya kwanza na pili, gharama zote zingine za masomo, ama kwa njia ya mkopo kutoka kwenye Bodi hii au kwa njia zake mwenyewe.

3.0. UREJESHWAJI WA MIKOPO

Kama ilivyobainishwa hapo juu, jukumu mojawapo la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ni kuhakikisha kwamba mikopo yote ambayo serikali ilitoa kwa wanafunzi waliosoma katika taasisi za elimu ya juu ndani au nje ya nchi kuanzia mwaka 1994/95 mpaka sasa inarejeshwa kwa wakati ili fedha hizo ziweze kutumika kuwakopesha wanafunzi wahitaji wengine.

Selikali ilitoa mikopo hiyo kwa wanafunzi kwa kuweka bayana kwamba fedha walizopewa ni mikopo na wala sio msaada au ruzuku na kwamba mikopo hiyo inapaswa ianze kurejeshwa mara baada ya mdaiwa kuhitimu masomo yake au pindi atakapositisha masomo yake kwa sababu mbalimbali.

4.0. MIKOPO ILIYOTOLEWA KATI YA MWAKA WA MASOMO 1994/95 MPAKA 2005/06

Kuanzia mwaka wa masomo wa 1994/95 mpaka 2004/05 mikopo ilitolewa kwa wanafunzi kwa ajili ya kugharamia chakula na malazi tu, lakini kuanzia mwaka 2005/06 mpaka sasa, pamoja na gharama ya chakula na malazi, wanafunzi wanakopeshwa pia fedha kwa ajili ya kugharamia ada ya mafunzo, vitabu na viandikwa, mafunzo kwa vitendo, mahitaji maalum ya vitivo na gharama za utafiti.

4.0 WAJIBU WA MDAIWA NA MWAJIRI KUHUSU UREJESHWAJI WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu, watu wote walionufaika na mikopo ya elimu ya juu pamoja na waajiri wa wadaiwa wanawajibu wa kuisaidia serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuhakikisha kwamba mikopo iliyotolewa kwa waliokuwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu inarejeshwa kwa wakati uliopangwa.

4.1 Wajibu wa Mdaiwa

Kwa mujibu wa kifungu cha 19 (1) cha sheria No. 9 iliyoanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ni wajibu wa kila mtu aliyenufaika na mikopo ya elimu ya juu kurejesha mkopo serikalini kupitia Bodi ya mikopo.

4.1.1 Mdaiwa aliyeajiriwa

  • Mdaiwa anapaswa kuitaarifu Bodi ya Mikopo ya Wanafuzni wa Elimu ya Juu kwa maandishi akionyesha anuani ya mwajiri wake wa sasa na atakayefuata (endapo atabadilisha kazi), Cheo chake, jina alilotumia chuoni, Chuo alichohitimu, kozi aliyohitimu na mwaka aliohitimu ili Bodi iweze kumpa maelezo sahihi ya mkopo wake na jinsi atavyolipa deni.
  • Mdaiwa anawajibika kuhakikisha kwamba makato yanayofanyika kwenye mshahara wake yanawasilishwa katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa wakati.
  • Pamoja na kukatwa marejesho ya mkopo kwenye mshahara wake, mdaiwa anaweza kuweka kiasi chochote cha fedha kwenye account ya bodi ikiwa ni marejesho ya mkopo wake. Mara baada ya kufanya hivyo anapaswa kuwasilisha "Bank deposit slip" katika Bodi ya mikopo ili aweze kurekebishiwa salio la mkopo wake.

4.1.2 Mdaiwa aliyejiajiri

  • Mdaiwa aliyejiajiri anawajibika kuiandikia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu akionyesha jina alilotumia chuoni, Chuo alichohitimu, kozi aliyohitimu mwaka aliohitimu, aina ya biashara aifanyayo, na mahali biashara ilipo.
  • Mara baada ya kupata taarifa za mdaiwa Bodi itampa maelezo yahusuyo deni lake na namna ya kulipa deni.

4.1.3 Mdaiwa asiyeajiriwa wala kujiajiri

  • Mdaiwa anawajibika kuitaarifu Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa maandishi jina alilotumia akiwa chuoni, Chuo alichohitimu, kozi aliyohitimu, mwaka aliohitimu, anuani yake na namba yake ya simu
  • Mara baada ya kupata taarifa za mdaiwa Bodi itampa maelezo yahusuyo deni lake na kujadiliana naye jinsi atakavyolipa deni.
  • Endapo mdaiwa atashindwa tulipa deni lake atashtakiwa kwa mujibu wa sheria. Na endapo atachelewa kuanza kulipa deni lake atapewa adhabu ya ongezeko la asilimia 10 ya mkopo wake.

4.2 Wajibu wa mwajiri

Kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1) cha sheria No. 9 iliyoanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ni wajibu wa kila mwajiri aliyeajiri mtumishi aliyenufaika na mikopo ya elimu ya juu, kuiarifu Bodi ya Mikopo na kutoa maelezo sahihi yahusuyo mwajiriwa yeyote ambaye alihitimu masomo ya Shahada au Stashahada ya juu kuanzia mwaka 1994 mpaka sasa na kuendelea kufanya hivyo pindi anapoajiri mtu wa namna hiyo kwa lengo la kuwatambua watu walio nufaika na mikopo hiyo.

Mara baada ya kupokea orodha ya waajiriwa walionufaika na mikopo na kiasi ambacho kila mmoja anadaiwa, Mwajiri anawajibika kisheria kukata marejesho ya kila mwezi kutoka kwenye mshahara au posho au mapato yoyote yale ya mwajiriwa ambaye amenufaika na mkopo na kuwasilisha marejesho hayo kabla ya tarehe 15 ya kila mwezi unaofuatia katika Bodi ya mikopo.

Mwajiri anayeshindwa kutoa taarifa za mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, atakuwa anatenda kosa na ataadhibiwa kwa kulipa faini ya shilingi millioni saba au kifungo kisichopungua miezi kumi na miwili au vyote kwa pamoja. Pale ambapo Mwajiri anaposhindwa kufanya makato kwenye mshahara wa mnufaika, ataadhibiwa kwa kulipa asilimia 10 ya kiasi cha marejesho ambayo yamecheleweshwa.

5.0 KIASI CHA MKOPO KINACHOHITAJIKA KUREJESHWA

Kwa sasa hivi mikopo ya elimu ya juu haina riba. Kwa sababu hiyo, aliyenufaika na mikopo hiyo anatakiwa kurejesha kile kiasi cha mkopo alichopewa bila riba.

6.0 NI WAKATI GANI MKOPO HUANZA KUREJESHWA?

Mdaiwa anapaswa kuanza kurejesha mkopo mara baada ya miezi kumi na miwili tangu tarehe ya kuhitimu masomo au mara baada ya kusitishwa/kusitisha masomo kwa sababu yoyote ile. Kwa mujibu wa sheria iliyounda Bodi ya mikopo, mkopo unapaswa urejeshwe ndani ya kipindi cha miaka 10.

7.0 ANUANI

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi kuhusu masuala yahusuyo urejeshaji mikopo, au maoni, tafadhali wasiliana na:-

Mkurugenzi Mtendaji,

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Plot No. 46, KSam Nujoma Road, Mwenge

S.L.P 76068

Dar es salaam

Simu: 022 2772432/33

Faksi: 022 2700286

Barua pepe: This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it

Tovuti: www.heslb.go.tz

 

Quote of The Day

Be Responsible; repay your higher education loan.

Higher Education Students' Loans Board