Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


29
February 2024

MPYA: MAOMBI YA MIKOPO STASHAHADA KUANZA KUPOKELEWA MACHI 1

Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wa Stashahada (Diploma) waliopata udahili wa kuanza masomo mwezi Machi, 2024 kuwa dirisha la kuomba mkopo kwa njia ya mtandao litafunguliwa kwa WIKI TATU kuanzia Machi 1, 2024 hadi Machi 22, 2024.

Wanafunzi wanapaswa kusoma ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada kwa mwaka 2023-2024 (TOLEO LA PILI)’ ambao unapatikana katika www.heslb.go.tz na www.nactvet.go.tz ili kufahamu kozi zinazopewa kipaumbele na utaratibu wa kuwasilisha maombi.

Kwa wanafunzi wa Stashahada waliodahiliwa awali na hawakuwa wamepata fursa ya kuomba mikopo, wanaruhusiwa pia kuomba mkopo kwa kuzingatia sifa na vigezo  vilivyoorodheshwa kwenye mwongozo.

MUHIMU: Wanafunzi waombaji wanasisitizwa kuzingatia muda wa kuwasilisha maombi (Machi 1 - 22, 2024) kwa kuwa hautaongezwa ili kutoa fursa ya uchambuzi na upangaji mikopo kwa wenye sifa.

 

Imetolewa na;

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

DODOMA

Alhamisi, Februari 29, 2024