4
Sep 2026

MTUHUMIWA WA KUFUTIA MADENI WANUFAIKA WA MIKOPO AKIRI KOSA

Mtuhumiwa wa kughushi na kujifanya mtumishi wa Bodi ya Mikopo sambamba na kuwalaghai wanufaika  kuwa anaweza kuwafutia mikopo, amekiri makosa na kuhukumiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, leo Ijumaa tarehe 4/9/2026.

Mtuhumiwa huyo Nicholaus Komba Mahitana aka Abdallah Mahimbo amehukumiwa kulipa faini ya Tzs. 1,600,000/=, kurejesha fedha taslimu Tzs 3,000,000/= pamoja na sharti la kuripoti katika kituo Kikiuu cha Polisi Mkoani Mbeya mara moja kwa mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu. Kesi hii imehitimishwa leo baada ya mtuhumiwa kumuandikia barua DPP akiomba kuridhia Mkataba wa kukiri makosa (Plea Bargaining).

Tukio hilo limeshuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  Dkt. Bill Kiwia, ambaye baada ya hukumu hiyo amewaasa wanufaika wa mikopo kufuata utaratibu sahihi wa urejeshaji na kuepuka kutumia vishoka ambao wanaweza kuwaingiza kwenye matatizo makubwa ikiwemo kupoteza ajira zao .

Published: September 4, 2026 at 3:31 PM