Frequently Asked Questions About Loans
HESLB loan application and allocation
Popular Questions
Zipi ni sifa kuu za kupata mkopo wa elimu ya juu?
- Awe mtanzania
- Awe ameomba mkopo kwa utaratibu ulioelekezwa (online)
- Awe amepata udahili (admission) kwenye chuo kinachotambuliwa na jina lake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo
- Asiwe na chanzo kingine cha kugharamia masomo yake ya chuo kikuu (mfadhili, ZHELB n.k)
- Maelezo ya kina kuhusu sifa na vigezo hutolewa na Mwongozo
Mkopo wa elimu ya juu unaombwaje?
- Maombi yote yanafanywa kwa njia ya mtandao wa Bodi ya Mikopo
- Kila mwombaji anapaswa kusoma kwa makini mwongozo unaotolewa ndani ya mwaka husika wa masomo
- Mwombaji atumie namba ya mtihani wa kidato cha nne kujisajili
Ni nyaraka gani muhimu zinatakiwa wakati wa kuomba mkopo?
- Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji kilichothibitishwa na RITA/ZCSRA
- Cheti cha kifo ikiwa umepoteza mzazi kilichothibitishwa na RITA/ZCSRA
- Kitambulisho cha mdhamini (NIDA, Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au Pasi ya Kusafiria)
- Fomu ya ufadhili iliyojazwa kwa usahihi ikiwa ulifadhiliwa katika masomo ya sekondari
- Barua ya Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa ikiwa mwombaji au mzazi wake ana ulemavu
- Picha (passport size) za mwombaji wa mkopo na mdhamini wake
Iwapo mwanafunzi/Mwombaji wa mkopo hajaridhika na kiwango cha mkopo alichopatiwa au hajapangiwa mkopo anatakiwa kufanya nini?
- Fursa ya kukata rufaa hutolewa baada ya kukamilisha zoezi la kupanga mikopo
- Ikitokea mwombaji akakosa kwenye rufaa, atapata fursa ya kuomba tena kwa mwaka unaofuata
General Questions
Mambo gani muhimu yanapaswa kuzingatiwa wakati wa kuomba mkopo?
- Hakikisha umesaini fomu ya maombi ya mkopo
- Hakikisha mdhamini wako amesaini fomu yako katika eneo lake
- Hakikisha fomu yako imesainiwa na kugongwa mihuri na Serikali ya Mtaa au Kijiji chako
- Hakikisha fomu yako imesainiwa na mwanasheria au hakimu kuthibitisha taarifa zako na za mdhamini wako
Mkopo unatolewa kwenye vipengele (Loanable Items) vipi?
- Chakula na malazi
- Ada ya mafunzo
- Vitabu na viandikwa
- Mahitaji maalumu ya kitivo
- Utafiti
- Mafunzo kwa vitendo
Nifanye nini ikiwa na nina swali kuhusu mkopo wa Elimu ya Juu?
- Taarifa zote kuhusu mikopo ya elimu ya juu hupatikana kupitia tovuti ya Bodi ya Mikopo
- Kwa wanafunzi waliopo vyuoni, kila chuo kina afisa anayesimamia masuala ya mikopo. Ulizia ofisi yake na atakuhudumia
Wajibu wa mwanafunzi mwenye mkopo akiwa chuoni ni upi?
- Kuwasilisha taarifa zake kwa afisa mikopo (Namba ya usajili na taarifa za benki)
- Kusaini malipo yanayotumwa chuoni kwake ndani ya muda uliopangwa
- Kutoa taarifa kwa afisa mikopo wa chuo chake mapema, kama kuna tatizo lolote linalohusiana na mkopo wake
- Kutembelea tovuti ya HESLB ili kupata taarifa mbalimbali za mikopo ya elimu ya juu