Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


16
June 2023

MUHIMU: KUANZA KWA USAJILI WA WANAFUNZI KATIKA 'DiDiS' ILIYOBORESHWA

Tunapenda kuwataarifu wanafunzi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuwa zoezi la kuwasajili wanafunzi katika mfumo wa kidijitali wa malipo (Digital Disbursement Solution – DiDiS) unatarajiwa kuanza Jumanne, Juni 20, 2023 kwa vyuo vilivopo jijini Dar es salaam.

Wanafunzi waliopo katika vyuo nje ya Dar es salaam

Kwa wanafunzi waliopo katika taasisi za elimu ya juu zilizopo nje ya Dar es salaam, usajili utafanyika kuanzia Juni 26, 2023. Taarifa zaidi zitatolewa kupitia kwa maafisa mikopo waliopo vyuoni na katika mitandao ya kijamii ya Instagram, Twitter na Facebook ya HESLB inayopatikana kwa jina la ‘HESLB Tanzania’.

DiDiS iliyoboreshwa

Mfumo wa DiDiS utakaotumika kuwasajili wanafunzi umeboreshwa kwa kujumuisha malipo ya ada ya mafunzo (Tuition Fee) moja kwa moja chuoni baada ya mwanafunzi kukiri kupokea fedha kupitia mfumo.

Aidha, wakati wa malipo, kwa wanafunzi wenye simu janja (smart phone) wataweza kupakua ‘HESLB App’ na kujihudumia popote pale walipo. Kwa wanafunzi wasio na simu janja, watapata huduma kupitia kwa Ofisa Mikopo aliyepo chuoni.      

Vitu anavyopaswa kuwa navyo mwanafunzi

Ili kusajiliwa, mwanafunzi anapaswa kufika katika eneo la usajili la chuoni kwake akiwa na kitambulisho cha uanafunzi, namba ya akaunti ya benki yenye majina yake na namba ya simu inayopatikana iliyosajiliwa kwa majina yake.

Aidha, HESLB inapenda kuwakumbusha wanafunzi na serikali za wanafunzi kutoa ushirikiano kwa maafisa watakaoendesha zoezi la usajili kama ilivyo kawaida.

Idadi ya wanufaika

Zoezi hilo linalenga kusajili wanafunzi waliopata mkopo kwa mara ya kwanza katika mwaka wa masomo 2022/2023 waliopo katika taasisi zote za elimu ya juu nchini. Mara baada ya usajili kukamilika, wanafunzi wote wanufaika wa mikopo waliopo vyuoni wapatao 202,016 watakua wanapokea fedha kupitia DiDiS.

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Jengo la PSSSF, Ghorofa ya Nne,

Barabara ya Makole,

S.L.P. 984,

DODOMA