Higher Education Students' Loans Board
215.3 BILIONI ZATOLEWA KWA WANAFUNZI 66,987
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Ijumaa, Novemba 7,2025 imetoa awamu ya pili ya upangaji mikopo na ruzuku yenye jumla ya wanafunzi 66,987. Idadi hii inajumuisha wanafunzi wafuatao:
i. Wanafunzi 43,562 wa shahada ya awali na wanafunzi 1,179 wa stashahada waliopangiwa mikopo kiasi cha TZS. 143.7 bilioni.
ii. Wanafunzi 288 wa Samia Skolashipu waliopangiwa ruzuku kiasi cha TZS. 575 millioni.
iii. Wanafunzi 230 wa Shule ya Sheria Tanzania waliopangiwa kiasi cha TZS. 1.5 bilioni.
iv. Wanafunzi 21,729 wanaoendelea na masomo wamepangiwa mkopo na ruzuku ya kiasi cha TZS. 69.4 bilioni baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliotangulia.
v. Mpaka sasa HESLB imekamilisha upangaji wa mikopo kwa wanafunzi 202,227 yenye thamani ya Shilingi 641.8 bilioni kati ya Shilingi 916.7 bilioni zilizotengwa na serikali kwa mwaka wa masomo 2025/2026.
Baada ya kukamilisha upangaji mikopo HESLB inawataarifu wanafunzi ambao hawajafanikiwa kupangiwa mikopo katika awamu zote mbili na wana taarifa za ziada ambazo hawakuweza kuziwasilisha wakati wa maombi ya mkopo wanashauriwa kukata rufaa. Dirisha la rufaa litafunguliwa tarehe 10 hadi 17 Novemba, 2025.
Maelekezo ya kukata rufaa yanapatikana katika akaunti binafsi ya mwombaji (SIPA).
HESLB itaendelea kupanga mikopo kwa wanafunzi wanaondelea na masomo kwa kadiri itakavyopokea matokeo kutoka vyuoni.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Jumatano, Novemba 07, 2025