Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


24
December 2020

Wanafunzi 2,009 wapangiwa mikopo ya TZS 6.02 bilioni dirisha la rufaa

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Alhamisi, Desemba 24, 2020) inawataarifu wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kuwa imetangaza orodha ya majina ya wanafunzi WAPYA 2,009 wa waliopangiwa mikopo yenye thamani TZS 6.02 bilioni.

Kundi hili, kama ilivyokua kwa wanafunzi wengine waliopangiwa mikopo katika awamu zilizopita, wamepangiwa kwa kuzingatia uhitaji wao na taarifa za ziada walizowasilisha na kuhakikiwa ipasavyo.

Hivyo, hadi sasa, jumla ya wanafunzi 55,287 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 179.17 bilioni katika awamu nne, ikiwemo hii iliyotangazwa leo. Kwa mwaka huu wa masomo 2020/2021, lengo lilikua ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 54,000.

“Wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kutembelea katika akaunti zao za SIPA walizotumia kuomba mkopo na watapata taarifa za kina kuhusu mkopo na matokeo ya rufaa”, amesema Mkurugenzi Mtendaji Abdul-Razaq Badru leo (Alhamisi, Desemba 24, 2020) jijini Dar es salaam.

Katika mwaka wa masomo 2020/2021, Serikali imetenga TZS 464 bilioni kwa ajili ya mikopo ya jumla ya wanafunzi 145,000. Kati yao, wanafunzi wa mwaka wa kwanza walitarajia kuwa 54,000 na wengine 91,000 ni wanaoendelea na masomo.

Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) na mitandao ya kijamii.

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Alhamisi, Desemba 24, 2020