RUFAA ZA MIKOPO SASA KUFUNGWA NOVEMBA 27, 2018

Kufuatia maombi ya wakata rufaa za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019, tunawajulisha wale wote wanaohitaji kukata rufaa na hawajakamilisha zoezi hilo kutokana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kutokamilisha nyaraka zinatohitajika, HESLB imeongeza siku mbili zaidi hadi Novemba 27, 2018.

Katika taarifa ya awali, dirisha la rufaa lilifunguliwa Jumatano, Novemba 21, 2018 na kuanza kupokea rufaa za mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kwa njia ya mtandao na ilitarajiwa lifungwe leo Jumapili, Novemba 25, 2018.

Wakata rufaa za mikopo ya Wanafunzi wanaweza kupitia https://olas.heslb.go.tz/  ambapo wanafunzi watakaotimiza masharti na sifa watapangiwa mikopo mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba, 2018.

Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM
JUMAPILI, NOVEMBA 25, 2018
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.