Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

 

MASWALI YAULIZWAYO MARA KWA MARA KUHUSU UREJESHAJI WA MIKOPO ELIMU YA JUU
  

Swali: Mwajiri anapaswa kufanya nini baada ya kuajiri wahitimu wapya?

  •  

Swali: Nini kitafuata baada ya kuwasilisha HESLB orodha ya wahitimu walioajiriwa?

Jibu: Baada ya kupokea orodha ya waajiriwa kutoka kwa mwajiri, Bodi itabainisha wafanyakazi walionufaika na mikopo ya elimu ya juu. Baada ya hapo, mwajiri atapaswa kuhakikisha kuwa makato ya kila mwezi kutoka kwenye mishahara ya wadaiwa wa mikopo yanawasilishwa Bodi ndani ya siku kumi na tano (15) baada ya tarehe ya kila mwisho wa mwezi.

 

Swali: Nini kitatokea endapo mwajiri ataacha kukata mshahara wa mfanyakazi baada ya kuelezwa na HESLB kwamba mfanyakazi huyo ni mdaiwa wa mkopo?

 

Jibu: Iwapo mwajiri atashindwa kukata ama kukata mshahara wa mdaiwa wa mkopo na kushindwa kuwasilisha makato hayo Bodi ndani ya muda uliopangwa, atatozwa asilimia kumi (10%) ya kiasi cha deni lililopaswa kulipwa kwa kila mwezi ambao makato hayatawasilishwa.

 

Swali: Ni lini mnufaika wa mkopo anapaswa kuanza kurejesha mkopo wake?

Jibu: Mkopo huanza kulipwa inapomalizika miezi 24 baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya juu au baada ya kusitisha masomo kwa sababu yoyote ile.

 

Swali: Je, ajira ya mdaiwa wa mkopo ni jambo linalozingatiwa katika urejeshaji wa mikopo?

Jibu: Wanufaika wote wa mikopo ya elimu ya juu wanapaswa waanze kurejesha mikopo mara baada ya miezi 24 baada ya kuhitimu. Lengo la muda huu ni kuwawezesha kutumia elimu waliyoipata kujiajiri au kuajiriwa na hivyo kupata kipato.

 

Swali: Ni asilimia ngapi hutozwa kama tozo la kutunza Thamani ya fedha kwa kila mdaiwa wa mkopo?

Jibu: Madeni yote ya mikopo hutozwa asilimia sita (6%) kama tozo la kutunza Thamani ya Fedha (Value Rention Fee) kwa mwaka.

 

Lengo la tozo hii ni kutunza thamani ya fedha dhidi ya mfumuko wa bei ili mkopo uwe na thamani sawa wakati utakapotolewa kwa mwanafunzi mwingine mwenye uhitaji katika siku zijazo.

 

Swali: Ni hatua zipi za kisheria zitachukuliwa kwa wadaiwa ambao hawatarejesha mikopo yao?

Jibu: Mdaiwa yeyote ambaye, bila sababu za msingi atashindwa kulipa mkopo atachukuliwa hatua za kisheria. Aidha, mambo yafuatayo yatafanyika:

 

  1. Atapata adhabu ya kulipa asilimia kumi (10%) ya mkopo wake wote;
  2. Taarifa zake zitawasilishwa kwenye taasisi zinazosimamia taarifa za wakopaji wanaotaka kukopa kutoka taasisi za fedha zinazotoa mikopo na kuzuiliwa kukopa kutoka kwenye Taasisi za Fedha;
  3. Atazuiliwa kupata ufadhili wa Serikali kwa ajili ya masomo ya Uzamili au Uzamivu katika chuo chochote cha Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi;
  4. Taarifa zao zinawasilishwa kwa wadau mbalimbali kama Mifuko ya hifadhi za Jamii ili hatua stahiki zichukuliwe;

 

Swali: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kampuni zingine binafsi za ukaguzi wana wajibu gani katika urejeshaji wa mikopo?

Jibu: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) na makampuni mengine binafsi ya Ukaguzi yana majukumu mawili:

  1. Kuhakikisha waajiri wanatekeleza matakwa ya Sheria kwa kuwasilisha orodha za wahitimu wa elimu ya juu walioajiriwa kwa Bodi ya Mikopo; na
  2. Kuhakikisha makato ya fedha kutoka kwa wadaiwa yanawasilishwa kwa wakati.

 

Swali: Mnufaika wa mkopo anapaswa kufanya nini ili kulipa deni lake?

Jibu: Mara baada ya kuhitimu masomo au kusitisha masomo yake kwa sababu yoyote ile, mnufaika anapaswa aitaarifu Bodi kwa maandishi mahali alipo na hali ya ajira yake na kuanza kurejesha mkopo wake.

 

Swali: Kwanini HESLB inatoa zawadi kwa waajiri wanaofanya vizuri katika kurejesha mikopo ya waajiriwa wao ambao ni wanufaika?

Jibu: HESLB inatoa zawadi kwa waajiri wanaofanya vizuri katika kurejesha mikopo ya waajiriwa wao ambao ni wanufaika ili kutambua mchango wao katika urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu na kujenga mahusiano mazuri na waajiri hao, vilevile inahamasisha waajiri wengine waweze kurejesha mikopo ya wanufaika waliowaajiri

 

Swali: Je ni waajiri wangapi hadi sasa wameshapata zawadi toka HESLB kwa kufanya vizuri katika urejeshaji wa mikopo?

Jibu: Jumla ya waajiri thelathini na saba (37); 15 kutoka Dar es Salaam, 10 kutoka Zanzibar na 12 kutoka kanda ya Arusha wameshapatiwa zawadi kwa kufanya vizuri katika urejeshaji wa mikopo

 

Swali: Makato huwasilishwaje HESLB?

Jibu: Kwa wanufaika waajiriwa, hukatwa asilimia kumi na tano (15%) ya mshahara wa kila mwezi.

 

Aidha, mnufaika anaweza kulipa kiwango cha chini cha shilingi 100,000/= kila mwezi kupitia Akaunti zifuatazo:


i. Benki ya Posta Tanzania CCA0240000032
ii. NMB Bank Akaunti 2011100205
iii. Benki ya CRDB Akaunti 01J1028467503



 

MASWALI NA MAJIBU YA UTOAJI MIKOPO

 

  1. Swali: Zipi ni sifa kuu za kupata mkopo wa elimu ya juu?

Jibu:

  • Awe mtanzania
  • Awe ameomba mkopo kwa utaratibu ulioelekezwa (online)
  • Awe amepata udahili (admission) kwenye chuo kinachotambuliwa na jina lake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo
  • Asiwe na chanzo kingine cha kugharamia masomo yake ya chuo kikuu (mfadhili, ZHELB n.k)
  • Maelezo ya kina kuhusu sifa na vigezo hutolewa na Mwongozo

 

  1. Swali:           Ninapaswa kufanya nini ili niweze kuanza kuomba mkopo kwa njia ya mtandao (OLAMS)?

 

Jibu:            Soma mwongozo unaotolewa na Bodi ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), kisha, fungua mtandao wa maombi (www.olas.heslb.go.tz) ili ujisajili kwa kutumia namba yako ya mtihani wa kidato cha nne na mwaka uliofanya mtihani huo.

 

  1. Swali:                    Baada ya kujisajili, napaswa kufanya nini?

Jibu:            Baada ya kujisajili, utapata namba ya kumbukumbu (Control Number) kwenye ‘screen’ ambayo itakuwezesha kufanya malipo ya ada ya maombi ya TZS 30,000/= kwa njia ya benki au simu. Lipa mara moja tu! Kiasi kamili cha TZS 30,000/=

 

                  Baada ya kulipa, utapokea ujumbe (sms) wa uthibitisho wa muamala wako utakaokuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ya maombi. Jaza hatua kwa hatua.

 

  1. Swali:          Ni nyaraka gani muhimu zinatakiwa wakati wa kuomba mkopo?
  2. Nakala za:
  1. Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji kilichothibitishwa na RITA
  2. Vyeti vya kidato cha IV & VI au Stashahada (Diploma)
  3. Cheti cha kifo ikiwa umepoteza mzazi kilichothibitishwa na RITA;
  4. Kitambulisho cha mdhamini (NIDA, Mpiga Kura; Leseni ya Udereva au Pasi ya Kusafiria). Mdhamini anaweza kutumia kimoja kati ya vitambulisho hivi.
  5. Barua ya taasisi mfadhili (Sponsor) ikiwa ulifadhiliwa katika masomo ya sekondari
  6. Barua ya Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa ikiwa mwombaji au mzazi wake ana ulemavu
  7. Picha (passport size) za mwombaji wa mkopo na mdhamini wake

(mdhamini anaweza kuwa mzazi au mlezi)

 

  1. Swali:          Je, iwapo nimehitimu kidato cha sita au diploma wa mwaka huu

wa masomo na sijapata cheti, nitaambatanisha nini?

 

Jibu:             Unatakiwa kujaza namba ya mtihani wa kidato cha sita ambayo itaweza kuhakikiwa na mamlaka husika. Kwa mhitimu wa diploma (Stashahada), unaweza kuambatanisha waraka wa matokeo (transcript).

 

         

  1. Swali:          Je, mwanafunzi anaweza kupata usaidizi wa kuomba mkopo

kwenye ‘Internet Café’?

jibu:

 

 

  1. Swali:          Je, nikijaza namba yangu ya mtihani isiyokuwa ya NECTA, kwa  

mfano ya nje ya nchi, nitawezaje kuendelea kuomba mkopo?

 

Jibu:            Wakati wa kujisajili, unatakiwa kuchagua kipengele cha ‘Non-NECTA students’ na kujaza kama inavyoelekezwa. Mfumo utakupatia namba ya kidato cha nne tofauti na ile uliyojaza ambayo itatambuliwa na mfumo wa Bodi. Namba hii mpya itatokana na taarifa yako ya namba uliyojazwa awali (isiyokuwa ya NECTA).

 

  1.  Inachukua muda gani fomu kufunguka baada ya kulipa?

 

Jibu:             Fomu inafunguka mara tu malipo yanapokamilika. Fomu inapochelewa kidogo kufunguka, mwombaji unashauriwa kutoka (Sign out) na kujaribu kuingia tena (Sign in) katika mtandao ili aweze kuendelea na hatua zinazofuata.

 

  1. Swali:          Ikiwa nimelipa lakini sijapokea ujumbe wa kuendelea na

maombi nifanyeje?

 

Jibu:             Unatarajiwa kupokea ujumbe mara tu muamala unapokamilika. Ikiwa hautapata ujumbe ndani ya saa moja (dakika 60) baada ya kufanya malipo, unashauriwa kuwasiliana nasi kwa namba ya simu +255 22 550 7910 au 0736 665 533 au barua pepe info@heslb.go.tz

 

  1. Swali: Nitafanyaje ikiwa njia mojawapo ya kulipia mfano, CRDB,

NMB,TPB, M-pesa, Airtel Money, Tigo-Pesa, T-Pesa itanigomea kulipa na kuendelea?

 

Jibu:             Kwa kuwa kuna njia zaidi ya moja ya kulipia, unashauriwa kutumia njia ya malipo ambayo ni rahisi kwako au inapatikana sehemu uliyopo wakati ukifanya malipo.

 

 

 

 

  1. Swali:          Nifanyeje iwapo nimesahau neno langu la siri (Password)?

 

Jibu:            Utapaswa kubofya kiunganishi cha “Forgotten the Password?” na kisha utapata neno jipya la siri hapo hapo (kwenye screen) mtandaoni.

 

  1. Swali:          Je, ni wapi nitahakiki cheti za kuzaliwa au kifo cha mzazi?

 

Jibu:             Vyeti vya kuzaliwa na vya vifo vya wazazi lazima vihakikiwe na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kabla havijapakiwa (uploaded) kwenye mtandao (olams)

 

  1. Swali:          Je kuna athari zozote ikiwa nimeambatanisha na kuwasilisha cheti ambacho hakijahakikiwa na RITA?

 

Jibu:             Ndiyo. Maombi yako yatakuwa hayajakamilika na hivyo kutofikiriwa katika hatua ya upangaji mikopo.

 

Unapaswa kuhakikisha nyaraka zote (siyo vyeti vya vifo au kuzaliwa tu) zinathibitishwa na mamlaka, taasisi au maafisa waliotajwa katika mwongozo.

 

  1. Swali:                    Kama simfahamu mzazi wangu, nitajaza nini?

 

Jibu:             Unatakiwa kujaza taarifa za mlezi au mtu mwingine anayekulea au kusimamia masuala yako ya Elimu. Ni lazima taarifa za mlezi au msimamizi zithibitishwe na Serikali ya Mtaa unakoishi. Kama mlezi anazo nyaraka rasmi za kukuasili (adoption document) nazo ziambatanishwe.

 

 

  1. Swali: Iwapo niliwahi kupata mkopo zamani na nikaacha, kushindwa                    au kufukuzwa chuo, nitaweza kupata mkopo mwingine?

 

Jibu:            Iwapo uliwahi kuwa mnufaika wa mkopo wa fedha za Serikali, utapaswa kwanza kurejesha mkopo wote au angalau asilimia 25 ya deni lako kabla ya kufikiriwa kupata mkopo mwingine. Deni unalopaswa kulipa utalipata kwenye mtandao (screen) na utatakiwa kulipa kwanza kabla ya kuendelea na maombi ya mkopo mpya.

 

  1. Swali:          Kama nina wazazi wasio na uwezo, je niwasilishe

 uthibitisho w aina gani ili kupata mkopo?

 

Jibu:             Mwombaji ambaye ana mahitaji maalum, ni lazima mahitaji na hali yake ithibitishwe na mamlaka husika kama Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi za aina hiyo. Taarifa za aina hii zitapekuliwa kuthibitishwa uhalisia na ukweli wake.

 

 

  1. Swali: Kama nilikosa mkopo mwaka jana, nikalazimka kuahirisha

masomo, natakiwa kuomba tena mkopo mwaka huu?

 

Jibu:             Unaruhusiwa kuomba upya mkopo mwaka huu. Maombi yako yatapimwa kwa mwongozo na vigezo vya mwaka huu wa masomo. Unashauriwa usome mwongozo kwa makini na kuuzingatia.

 

                  Aidha, kama unasoma mwaka wa pili au wa tatu na kuendelea na una uhitaji wa mkopo, unaruhusiwa kuomba kwa kuzingatia vigezo vya mwaka huu.

 

  1. Swali: Nitafanyaje nisipoweza kumfikia mtoa huduma kwa njia ya

Simu zinazoonyeshwa kwenye mtandao?

 

Jibu:            Kuna njia mbili za kuwafikia watoa huduma wa kitengo cha usaidizi (Helpdesk) Njia ya kwanza ni kwa simu +255 22 550 7910 au 0736 665 533 na nyingine ni kwa barua pepe info@heslb.go.tz.

 

Unashauriwa kuwasilisha taarifa au changamoto husika kwa njia ya barua pepe ili wataalamu waifanyie kazi na kukupigia simu kama itahitajika. Kumbuka kuandika mawasiliano yako ya simu itakayotumika kukupigia.

 

  1. Swali: Je, nitajuaje kama nimejaza fomu ya maombi kwa ukamilifu?

 

  •  
  1. Picha ya mwombaji na picha ya mdhamini wako;
  2. Vivuli vya nakala za vyeti vya kitaaluma zilizothibitishwa na Wakili au Mahakama;
  3. Vivuli vya nakala za vyeti vya kuzaliwa au kifo zilizothibitishwa na RITA;
  4. Nakala za barua za ufadhili kutoka katika taasisi zinazotambulika;
  5. Nakala ya kitambulisho cha mdhamini kilichothibitishwa na Wakili au Mahakama;
  6. Nakala ya fomu ya maombi iliyosainiwa na kugongwa muhuri na Serikali ya Mtaa, Mahakama au Wakili kama inavyoelekezwa;
  7. Aidha, nakala halisi ya fomu ya maombi inapaswa kusainiwa na mwombaji na mdhamini wake
  8. Maelezo ya kina yanapatikana katika mwongozo uliopo kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz)

 

  1.  Swali: Fomu za maombi ya Mikopo zinawasilishwaje Bodi ya Mikopo  ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu?

 

Jibu:            Baada ya kuzi-upload na kukamilisha kujaza fomu ya maombi, mwombaji a-print fomu iliyokamilika na kuituma kwa EMS kwenda kwa:

 

Mkurugenzi Mtendaji,

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,

Barabara ya Sam Nujoma – Mwenge

S.L.P. 76068

14113 DAR ES SALAAM

 

 

        

  1. Swali:                    Mwombaji atajuaje iwapo amepata mkopo?

 

Jibu:            Baada ya Bodi kupokea, kuhakiki na kuchambua maombi ya mikopo, majina ya Wanafunzi watakaofanikiwa kupangiwa mikopo yatatangazwa kupitia tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) kabla ya kufunguliwa kwa vyuo vya elimu ya juu walikodahiliwa Wanafunzi husika.

 

  1. Swali: Mkopo unatolewa kwenye vipengele (Loanable Items) vipi?

Jibu:           

  • Chakula na malazi
  • Ada ya mafunzo
  • Vitabu na viandikwa
  • Mahitaji maalumu ya kitivo
  • Utafiti

Mafunzo kwa vitendo

 

 

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

  •