Higher Education Students' Loans Board
1. Ingia kwenye tovuti (www.heslb.go.tz) ili kusoma orodha ya majina ya wanafunzi walengwa wa ‘SAMIA SCHOLARSHIP’ kwa mwaka 2023-2024;
2. Ingia (https://olas.heslb.go.tz) kujaza fomu ya ufadhili;
3. Bofya ‘Apply for Scholarship’;
4. Baada ya kitufe husika kufunguka, chagua ‘SAMIA SCHOLARSHIP’;
5. Jaza namba yako ya mtihani wa Kidato cha IV uliyotumia kuomba udahili (admission) chuoni;
6. Baada ya fomu kufunguka, thibitisha vitu vifuatavyo kwa kubofya ‘confirm & proceed to next step’;
i. Majina yako,
ii. Namba za mitihani ya Kidato cha IV na Kidato cha VI,
iii. Majina ya shule za Sekondari,
iv. Tahasusi na ufaulu
7. Hakikisha unazingatia yafuatayo;
i. Pakia picha ya mwombaji yenye vipimo vya 120x150 pixels’, size <1MB format jpg
ii. ‘Print’ fomu yako kwa kusainisha ukurasa wa pili
iii. Pakia ukurasa wa pili uliosainiwa kikamilifu kwenye mfumo
8. Kamilisha maombi yako kwa kubofya kitufe ‘submit your application’