Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


19
October 2022

HESLB YAANZA KUTOA ORODHA YA WANUFAIKA 2022/2023

Fedha za wanafunzi kutumwa vyuoni wiki hii

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Jumatano (Oktoba 19, 2022) imeanza kutangaza wanafunzi wahitaji waliopangiwa mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo 2022/2023.

Wanafunzi kupata taarifa kupitia SIPA

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema wanafunzi wote walioomba mkopo kwa mwaka 2022/2023 wanaweza kupata taarifa za kina kupitia akaunti walizotumia kuombea mikopo maarufu kama ‘SIPA’ - Student’s Individual Permanent Account.

“Leo tumeanza kutoa ‘updates’ kwa makundi yote, waliopangiwa mikopo, ambao bado tunaendelea kufanyia kazi na wale wanaotakiwa kufanya marekebisho … kila mmoja anapata taarifa yake kwenye akaunti ile ile aliyotumia kuomba mkopo, huhitaji kufika ofisini kwetu” amesema Badru.

Katika hatua nyingine, Badru amesema HESLB imeanza kuandaa malipo ya wanafunzi wapya na wanaoendelea na masomo ambao ni wanufaika wa mikopo na kusema lengo ni kuhakikisha fedha zinafika vyuoni kwa wakati.

Fedha imepokelewa, kuanza kuwafikia wanafunzi vyuoni wiki hii

“Mwaka huu, kama miaka iliyopita, fedha inayohitajika kwa ajili ya mahitaji ya wanafunzi ya muhula wa kwanza imepokelewa, … tunakamilisha uandaaji wa malipo ya muhula wa kwanza, na fedha zitaanza kuwafikia wanafunzi katika vyuo vya mwishoni mwa wiki hii,’ amesema Badru.

Wito: Vyuo kuwasilisha matokeo ya mitihani

Kuhusu wajibu wa vyuo, Badru amevikumbusha vyuo ambavyo havijawasilisha matokeo ya mitihani ya wanafunzi-wanufaika wanaoendelea na masomo, kuwasilisha ili kuiwezesha HESLB kuandaa malipo kwa wakati.

“Kuna vyuo vichache, kama 11 ambavyo bado havijawasilisha matokeo, tumewakumbusha na tunasisitiza waharakishe kuwasilisha matokeo ili tukamilishe malipo ya wanafunzi waliofaulu kuendelea na masomo,” amesema Badru.

Imetolewa na:

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Dar es salaam, Jumatano, Oktoba 19, 2022