![]() |
|
![]() |
Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu maoni yaliyotolewa na wadau wetu mbalimbali kupitia vyombo vya habari vya jana (Jumanne, Februari 2, 2021) na leo (Jumatano, Februari 3, 2021) kuhusu makato na tozo katika urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu.
Kupitia maoni hayo, pamoja na mambo mengine, wadau wetu wamezungumzia viwango vya makato na tozo ambazo tumeona ni vema kutoa ufafanuzi wa viwango sahihi ili kuongeza uelewa wa wateja wetu na wananchi kwa ujumla kama ifuatavyo:
Baada ya kuwasilishwa HESLB, fedha hizo huingizwa katika akaunti ya mnufaika ili kupunguza deni lake, kulipa tozo mbili au tatu kulingana na deni la mnufaika – wapo wenye adhabu kwa kuchelewa kuanza kurejesha na wapo wasio na adhabu.
Lengo la tozo hii ni kuiwezesha Serikali, kupitia HESLB, kuwa na mfuko endelevu utakaowezesha kukopesha wahitaji wengine bila kuathiri thamani ya fedha za mkopo ambazo mnufaika alipokea akiwa masomoni.
Tunapenda kuwakumbusha wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajajitokeza, kujitokeza na kuanza kurejesha ili kuepuka adhabu na kumaliza madeni yao ili wahitaji wengine wanufaike.
Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Dar es salaam
Jumatano, Februari 3, 2021