The United Republic of Tanzania
HIGHER EDUCATION STUDENTS' LOANS BOARD

UFAFANUZI WA TAARIFA ZINAZOSAMBAA MITANDAONI


Tunapenda kuwajulisha waombaji mkopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021 kuwa HESLB bado haijatoa orodha ya wanafunzi waliopangiwa mkopo. Kwa sasa, kazi ya uchambuzi wa maombi ya mkopo yaliwasilishwa inaendelea.

Taarifa hii inafuatia kuwepo kwa taarifa zisizo sahihi ambazo zinasambazwa mitandaoni kuwa HESLB imetangaza orodha ya waanafunzi ambao wamepangiwa mkopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

Aidha, taarifa hizo zisizo sahihi zinaelekeza waombaji mkopo kupakua mfumo (application) katika simu zao utakaowawezesha kuona orodha ya wanafunzi waliopangiwa mkopo kwa mwaka 2020/2021.

Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi waombaji wa mkopo na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo sio sahihi na hazijatolewa na HESLB na zipuuzwe.

Taarifa rasmi kuhusu HESLB, zikiwemo zinazohusu wanafunzi wanaopangiwa mkopo zitatolewa kuanzia Novemba 10, 2020 kupitia akaunti walizotumia kuomba mkopo (SIPA – Student’s Individual Permanent Account).

Taarifa pia zitatolewa kupitia vyombo vya habari, tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) na mitandao ya kijamii ya HESLB ambayo ni twitter, instagram na facebook kwa jina la ‘HESLB Tanzania’.

 

Imetolewa na:

 

Abdul-Razaq Badru

Mkurugenzi Mtendaji

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Jumatatu, Oktoba 19, 2020