The United Republic of Tanzania
HIGHER EDUCATION STUDENTS' LOANS BOARD

TAARIFA MUHIMU: MASAHIHISHO YA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020


HESLB imeongeza muda wa siku mbili kwa waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ambao fomu zao zilibainika kuwa na upungufu ili wakamilishe marekebisho hayo hadi Jumapili Oktoba 6, 2019 saa 5.59 usiku.

Nyongeza ya muda wa marekebisho inalenga kuwapatia fursa waombaji wanaotakiwa kufanyia marekebisho fomu zao za maombi na ambao kwa kufunga mfumo leo Oktoba 4, 2019 iliyokuwa tarehe ya mwisho kwa mujibu wa tangazo la Septemba 29, 2019; hawataweza kukamilisha.

Hadi kufikia leo Oktoba 4, 2019, kati ya wanafunzi 10,571 ambao fomu zao za maombi zilibainika kuwa na upungufu, waombaji 7,558 wamekamilisha kufanya marekebisho, idadi ambayo ni sawa na 71.6%. Idadi iliyobaki ya waombaji mikopo 3,013 (28.4%) ndio ambao hawajakamilisha masahihisho.

Hatua ya HESLB kuwaita baadhi ya waombaji mikopo kufanya masahihisho kwenye fomu zao inafuatia kukamilika kwa uhakiki wa maombi ya mikopo ambapo ilibainika baadhi ya fomu za maombi ya mikopo zina upungufu unaozuia kuendelea na hatua ya kupangiwa mikopo.

Upungufu huo ni pamoja na kukosa nyaraka ama viambatanisho vilivyothibitishwa na mamlaka husika na saini za waombaji na wadhamini wao.
 

  • Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shahada ya kwanza *bofya hapa.*
  • Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shule ya Sheria (Law School of Tanzania) *bofya hapa.*
  • Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shahada za Uzamili na Uzamivu*bofya hapa.*


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
04 Oktoba 2019