Kwa mujibu wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (SURA 178), mwajiri anapaswa aijulishe Bodi kwa maandishi kuhusu waajiriwa wapya ambao ni wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu ndani ya siku ishirini na nane (28) tangu tarehe ambayo wahitimu hao wameajiriwa
Mara baada ya kuhitimu masomo au kusitisha masomo yake kwa sababu yoyote ile, mnufaika anapaswa aitaarifu Bodi kwa maandishi mahali alipo na hali ya ajira yake na kuanza kurejesha mkopo wake.