| TAARIFA KWA WAOMBAJI WA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013 |
|
1. 0 FURSA YA MWISHO KWA WANAFUNZI WANAOENDELEA NA MASOMO AMBAO HAWAKUJAZA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO KUJAZA FOMU HIZO Uchambuzi wa maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2012/2013 umebaini kuwepo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo na wale wanaoomba kwa mara ya kwanza ambao hawakujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao (OLAS) na pia kutowasilisha fomu za ombi.
Bodi imetoa fursa ya mwisho kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo kukamilisha maombi ya mikopo katika kipindi cha siku kumi na nne, kuanzia tarehe 18 Julai, 2012 kupitia mtandao kwa anuani: http://olas.heslb.go.tz. Aidha Wanafunzi wanaoendelea na masomo watakaotuma maombi yao wanatakiwa kulipa faini ya Tsh. 30,000/= kwa njia ya M-Pesa. Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi hayo ni 31 Julai 2012. Hakutakuwa na muda wa ziada baada ya muda huo kupita. 2. 0 KUWASILISHA FOMU ZA WAOMBAJI WAPYA Bodi pia inawataarifu waombaji wote wa mikopo wa mara ya kwanza ambao hawakuwasilisha fomu zao kwa wakati kutumia muda huu wa wiki mbili kuwasilisha fomu zao Bodi zikiwa na viambatanisho vinavyohitajika. Aidha hakutakuwa na muda wa ziada wa kuwasilisha fomu hizo baada ya tarehe Julai 31, 2012.
3.0 HITIMISHO Waombaji ambao hawakukamilisha taratibu za maombi ya mikopo wanahimizwa kutekeleza maelekezo haya ndani ya muda uliopangwa kama ilivyoelekezwa. Baada ya muda huo kuisha hakutakuwa na muda wa ziada na hivyo watakaoshindwa kutekeleza hawataweza kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2012/2013.
IMETOLEWA NA: KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
|