WANAOREJESHA WATAKIWA KUONGEZA TAARIFA ZA UTAMBULISHO

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawapongeza wanufaika wote wa mikopo ambao wanarejesha mikopo yao iliyoiva ili kuwawezesha wengine wanufaike.

 

Hata hivyo, HESLB imegundua kuna baadhi ya wanufaika ambao wanarejesha mikopo lakini taarifa zao haziko kamili na hivyo Bodi kushindwa kuhuisha taarifa za madeni yao.

 

Kwa taaifa hii, HESLB inapenda kuwataarifu wanufaika hao ambao majina yao yanapatikana kwenye orodha ya kwanza iliyoko kwenye tovuti hii kuwa kila aliyeorodheshwa anapaswa kuongeza taarifa zifuatazo:

 

-          Nambari ya mtihani wa Kidato cha Nne (Form Four Index Number) na mwaka aliomaliza kidato cha nne

-          Jina kamili lililotumika elimu ya juu

-          Jina la taasisi ya elimu ya juu alikohitimu

-          Mwaka wa kuanza na mwaka wa kuhitimu  elimu ya juu

 

Pakua orodha ya Wanaorejesha

Taarifa hizo zitumwe kwa njia ya barua pepe kwa anuani zifuatazo:

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.  au This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 

Iwapo una swali au unahitaji ufafanuzi zaidi wasiliana nasi kwa simu ya mkononi:

0621 870 172

 

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu