SALAMU ZA MWAKA MPYA 2017

Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu wanawatakia wadau wake wote heri ya mwaka mpya 2017 kwa ahadi ya kuendelea kuboresha huduma za utoaji na urejeshwaji wa mikopo kwa wanufaika.

Kila mwaka Bodi inaendelea kubuni mikakati makini ya kuhakikisha utoaji na urejeshwaji wa mikopo unakuwa wa ufanisi zaidi kwa kuwahusisha wadau wake muhimu.

Pamoja na salamu hizo, Bodi inaendelea kuwakumbusha wanufaika wa mikopo ambao wamehitimu masomo kwenye vyuo vya elimu ya juu kuanzia miaka miwili iliyopita na kuendelea na ambao hawajaanza kurejesha, kuanza na kuendelea kurejesha mikopo yao.

Kwa vile madeni yao yameiva muda mrefu na kugeuka kuwa wadaiwa sugu;  wafanye yafuatayo:

(i) Wajitokeze kabla picha zao hazijatolewa kwenye vyombo vya habari.

(ii) Ambao wamo kwenye orodha ya wadaiwa sugu na tayari wamelipa Benki lakini Bodi haina taarifa; wawasilishe stakabadhi za malipo hayo ofisi za Bodi kwa ajili ya kuweka sawa kumbukumbu.

Mwaka 2016 umemalizika kwa Bodi kutoa huduma za taarifa za madeni kwa wadaiwa sugu kwa muda wa siku 46 na zoezi linaendelea kwa kuongeza mikakati.

Ni wajibu wa kila mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu kurejesha mkopo ili kuwanufaisha wahitaji wengine.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

01/01/2017