WASUGU KUHUDUMIWA IJUMAA, JUMAMOSI NA JUMAPILI

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya zoezi la kuwataka wadaiwa sugu kulipa madeni yao ndani ya siku 30, Ofisi za Bodi ya Mikopo zilizopo Mwenge, jijini Dar es Salaam zitakuwa wazi kwa siku tatu, Ijumaa, Disemba 09, 2016,  Jumamosi, Disemba 10, 2016 na Jumapili, Disemba 11, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri ili kutoa fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao kupata taarifa kuhusu madeni yao na kulipa.

Njoo na Majina yako kamili, Chuo ulichosoma, Mwaka wa kuanza na wa kuhitimu, anuani yako ya barua pepe (email), nambari ya simu yako ya kiganjani, mwajiri wako na Check Number yako iwapo umeajiriwa serikalini.

Nyote mnakaribishwa ili kutumia fursa hii muhimu kabla ya zoezi kuhitimishwa na hatua za kisheria kuanza kuchukuliwa.

‘Kuwa Mzalendo, Rejesha Mkopo wa Elimu ya Juu’

Kwa mawasiliano zaidi piga 0767 513208
 

Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
08/12/2016