Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


30
November 2020

WANAFUNZI WAPYA 5,168 WAPANGIWA MIKOPO YA TZS 19.9bn

Jumanne, Novemba 17, 2020

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawajulisha waombaji wa mikopo na wadau wengine kuwa imetoa orodha ya Awamu ya Pili yenye wanafunzi 5,168 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 19.9 bilioni.

Itakumbukwa kuwa Novemba 11, 2020, HESLB ilitangaza orodha ya Awamu ya Kwanza iliyokuwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 47,305 waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 150.03 bilioni.

Hivyo, hadi leo (Jumanne, Novemba 17, 2020), jumla ya wanafunzi 52,473 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mkopo yenye thamani ya TZS 170.02 bilioni.

Wanafunzi wanatakiwa kutembelea katika akaunti zao za SIPA walizotumia kuomba mkopo na watapata taarifa za kina kuhusu mkopo.

Waliokosea sasa ruksa kurekebisha

Kuhusu wanafunzi waombaji ambao maombi yao yana upungufu, HESLB imewapa siku tano (05) kuanzia kesho (Jumatano, Novemba 18, 2020) kurekebisha taarifa zao kwa njia ya mtandao.

Hivyo, kuanzia kesho wataweza kuingia katika akaunti zao za SIPA walizotumia kuomba mkopo na kurekebisha kwa kuweka nyaraka sahihi na HESLB tutazifanyia uchambuzi na wenye sifa watapangiwa mikopo mapema iwezekanavyo.

Bajeti ya Mikopo 2020-2021

Katika mwaka 2020/2021 Serikali imetenga TZS 464 bilioni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi 145,000. Kati yao, wanafunzi 54,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza na 91,000 ni wanafunzi wanaoendelea na masomo. 

 

Imetolewa na:

Abdul-Razaq Badru

Mkurugenzi Mtendaji

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu