Higher Education Students' Loans Board

  • Dar es Salaam, Tanzania. P.O.Box 76068

  • General call +255 22 286 4643

  • Monday - Friday8:00am - 5:00pm

News & Events


29
May 2020

HESLB: Tumeshalipa TZS 63.7 bilioni kwa vyuo 81

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru amesema tayari taasisi yake imeshatuma TZS 63.7 bilioni kwenye vyuo na taasisi za elimu 81 kwa ajili ya malipo ya fedha mkopo wa chakula na malazi kwa jumla ya wanafunzi 132,119 wanaotarajia kuanza masomo keshokutwa, Juni 1.

“Hadi jana, Mei 28, 2020, jumla ya TZS 63.7 bilioni zilikua tayari vyuoni kwa ajili ya malipo fedha za chakula na malazi kwa robo ya tatu yam waka wa masomo 2019/2020 na tumevieleza vyuo kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wanafunzi kama ilivyokusudiwa na Serikali,” amesema Badru leo (Ijumaa, Mei 29, 2020) jijini Dodoma katika mkutano na wanahabari.

Mkutano huo ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kuhudhuriwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Faustine Bee, wawakilishi wa viongozi wa wanafunzi walioongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini (TAHLISO, Peter Niboye na Rais wa Serikali ya Wanafunzi UDOM, Godfrey Mwamwenge.

Akizungumza mkutano huo, Prof. Bee amesema chuo chake kimepokea kimepokea fedha za wanafunzi na tayari kimeanza kuwapokea wanafunzi kuanzia leo, Mei 29 na taratibu za kuwasajili na kuwalipa fedha zinaendelea. Kwa upande wake, Niboye amewakumbusha wanafunzi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kufika vyuoni, kusaini nyaraka muhimu ili kupkea fedha kwa wakati kama inavyoelekezwa na Serikali kupitia HESLB na vyuo.

“Sisi kama TAHLISO tunaishukuru Serikali kwa kufungua vyuo na kutoa fedha haraka, lakini tunawahimiza wanafunzi wote kufika vyuoni, na wale wenye mikopo kutimiza wajibu wao wa kusaini … hatutakua tayari kupokea malalamiko yanayotokana na wanafunzi kutotimiza wajibu wao,” amesema.